Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – TARURA, kuacha utaratibu wa kuchimba barabara na kuziacha na mashimo kwa muda mrefu bila kuyafukia.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo na kuwataka Mameneja wa TARURA kuhakikisha kuwa bajeti ya kufukia mashimo inakuwepo pale ambapo wanakwenda kuchimba mashimo katika barabara.

Aidha, pia ameonya kuwa atawaondoa katika nafasi zao watendaji wa TARURA pamoja na Mameneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya pale ambapo mashimo hayo yataachwa wazi hadi wiki mbili bila kuyafukia kwa utaratibu unaofaa.

Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amesema yapo mashimo yamechimbwa na kuachwa wazi kwa mwezi mzima, hali inayosababisha adha kwa watumiaji wa barabara na wakati mwingine kusababisha ajali.

Mradi wa Bil. 42 kusaidia uvutaji Maji Ziwa Victoria
Watakiwa kutunza mradi uhimili mabadiliko Tabianchi