Lydia Mollel – Morogoro

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro, SSP Denis Mujumba amewataka Waendesha Pikipiki maarufu kama Bodaboda kuacha tabia ya kuwalaghai Wanafunzi, kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wamefanya kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mujumba wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kwa Madereva wa Vyombo vya Moto, yatakayofanyika Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro, yakilenga kuwapa elimu ili kupunguza ajali za barabarani na kulinda usalama wa Wananchi.

Awali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kata ya Lukobe, Zuwena Mwita alisema kupitia mafunzo hayo wanatarajia Wanafunzi hao kujiepusha na matukio ya kiuhalifu, kwani watakuwa wamepata elimu ya kutosha, kutambua sheria na taratibu zinazowapasa kuishi nazo na kuwa raia wema.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro, SSP Denis Mujumba.

Kwa upande wao Wananchi, wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuelewa Sheria za Barabarani, kujua namna ya kusaidika katika mambo mbalimbali ya kijamii na kujiepusha na vitenndo vya uvunjaji wa sheria ambazo hapo awali hawakuwa na uelewa nazo.

Mafunzo hayo, yamelenga kutoa elimu mbalimbali ikiwemo dhana ya Polisi Jamii, elimu ya maendeleo ya jamii, ukatili wa kijinsia, makosa kwa njia ya mtandao, umuhimu wa chombo cha moto, jinsi ya kupata Tin namba namba na kubadilisha Kadi ya Vyombo vya Voto, kupata utambulisho wa uraia, lesseni na usafirishaji.

Tanzania yaongoza kampeni AFCON 2027
Kennedy Juma asukwa kuivaa Power Dynamos