Nahodha na Beki wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Young Africans, Bakari Nondo Mwamnyeto amewaita mashabiki wa timu hiyo kuja uwanjani kwenye mchezo wao wa Mkondo wa Pili wa Raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh.

Young Africans itakuwa wenyeji wa Al Merreikh Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es salaam ikiwa ni baada ya majuma mawili kwa wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Pele, Kigali, Rwanda.

Mabao ya Youybg Africans kwenye mchezo huo yalifungwa kipindi cha pili na washambuliaji wake mahiri Kennedy Musonda na chipukizi Clement Mzize.

Mwamnyeto aliyeukosa mchezo wa awali kutokana na kuomba udhuru ya kumuuguza baba yake mzazi aliyeugua ghafla Tanga, tayari amejiunga na wenzake na kuwaomba mashabiki wa timu hiyo kufurika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuishangilia timu yao kwenye mchezo huo muhimu ambapo kama Young Afracas watatoka sare au kupata ushindi wa aina yoyote wataingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

“Jumamosi tunawaomba mashabiki wetu waje uwanjani kwa wingi, sisi tutapambana kuhakikisha tunawapa furaha,” amesema Mwamyeto kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo.

Young Africans wanakaribia kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1998 kwa kuitoa Coffee ya Ethiopia, ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Addis Ababa timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kabla ya kuja kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 Uwanja wa Uhuru.

Erasto Nyoni afichua mipango Namungo FC
Mlipuko homa ya Denge, Kipindupindu wauwa, hofu yatawala