Nahodha na Kiungo wa KMC FC, Awesu Awesu amesema ushindi walioupa dhidi ya JKT Tanzania umewaongezea ari ya kufanya vizuri katika mechi zijazo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, mchezaji huyo amesema pamoja na ushindani mkubwa uliopo msimu huu, lakini wamejipanga kukabiliana nao.

“Ni kweli ushindani msimu huu ni mkubwa, lakini sisi KMC tunafurahia sababu tuna timu nzuri yenye kumudu ushindani uliopo,” amesema Awesu.

Kuhusiana naa malengo ya KMC msimu huu, nahodha huyo amesema wanataka angalau kuwepo kwenye natasi tano za juu kama ilivyokuwa kwenye msimu wao wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema kuwaza ubingwa kwa sasa ni ngumu kutokana na ubora waliokuwa nao Simba SC, Young Africans na Azam FC, ndio maana wamejiwekea malengo hayo.

Awesu amesema vita yao kubwa msinu huu itakuwa dhidi ya timu za daraja la kati ambazo wanalingana kiuwezo.

Ushindi dhidi ya KMC unaiweka timu hiyo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na ponti sita na mabao matatu.

Kibu Denis aahidi furaha Azam Complex
Erasto Nyoni afichua mipango Namungo FC