Bondia Hassan Mwakinyo ambaye ilibidi acheze pambano la kuwania mkanda wa IBA Intercontinental dhidi ya Rayton Okwiri sasa amebadilishiwa mpinzani.

Katika pambano hilo la raundi 10 litafanyika jijini Dar es salaam keshokuwa Ijumaa (Septemba 29) na sasa atazichapa dhidi ya Julius Indongo kutoka Namibia.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Mwakinyo ameandika: ” Binafsi sijaridhishwa na mabadilko hayalakini ni bora kugawa chakula kilichokwisha andaliwa kuliko kutupa, natumai washabiki zangu ni waungwana na kwa pamoja mtaelewa mabadiliko haya,”

Usambazaji Umeme Vijijini kukamilika Desemba
Nasser Al-Khelaifi: Messi asiudanganye umma