Afisa Tarafa wa Sisimba, John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu na kutowaruhusu wanafunzi kushiriki kwenye sherehe za usiku lakini pia kukenea utoro katika baadhi ya shule zinazopatikana ndani ya kata hiyo.

Mboya ameyaeleza hayo akiwa katika ziara zake za kupitia na kukagua hali ya taaluma katika kata hiyo na kugundua kuwepo kwa utoro na wazazi kutowasimamia kielimu, hali inayoweza kupelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Ziara hiyo inalenga kutatua changamoto zilizopo katika suala la elimu kata ya Itagano ilyopo Tarafa ya Sisimba na kuzungumza na watumishi waliopo katika kata hiyo.

Lomalisa hatarini kuikosa Al Merreikh
Urembo uliopitiliza ni ukatili kwa watoto