Endapo ulikuwa sehemu ya Mashabiki wa Soka waliodhani Harry Kane tayari ana hat trick moja katika Ligi ya nchini Ujerumani ‘Bundesliga’, basi ulikosea sana, kufuatia sheria za ligi hiyo kumnyima Mshambuliaji huyo kuwa na hat trick licha ya kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja.

Kane ambaye amejiunga na Bayern Munich msimu huu, mwishoni mwa juma lililopita alifunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Bochumn, akifunga dakika ya 12, 54 na 88.

Sheria za Bundesliga zinasema kwamba, ili ihesabike umefunga hat trick, lazima mabao yote matatu uyafunge katika kipindi kimoja cha mechi, huku pia ufunge mabao mfululizo, bila ya mchezaji mwingine wa timu yako kuingilia katikati yake.

Ukiangalia namna Kane alivyofunga, alifunga bao moja kipindi cha kwanza, mawili kipindi cha pili. Lakini pia hayakuwa kwa mfuatano.

Katika mchezo huo, mabao mengine yalifungwa na Erik Maxim Choupo-Moting (dk 8), Matthijs de Light (dk 29), Leroy Sane (dk 38) na Mathys Tel (dk 81).

Kane tangu ajiunge na Bayern, amekuwa na wakati mzuri ambapo amefunga mabao nane na asisti nne katika mechi sita za michuano yote.

Licha ya hat trick hiyo kutotambulika na Bundesliga, lakini katika mchezo huo, Kane alikabidhiwa mpira kama inavyokuwa utaratibu kwa mchezaji kukabidhiwa akipiga hat trick.

Yusuph Dabo: Hatutarudia makosa Ligi Kuu
Shomari Kapombe awajibu wanaombeza