Boniface Gideon – TANGA.

Maonesho ya Biashara yanayoshirikisha Wanawake Wajasiriamali maarufu kama Tanga Woman Gala msimu wa sita, yamezinduliwa rasmi jijini Tanga, mbapo zaidi ya Wafanyabiashara 100 kutoka maeneo Mbalimbali nchini wamepata fursa ya kuonyesha bidhaa zao.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Five Brothers ambao ndio waandaji wa Maonesho hayo, Nassor Makau amewaambia Waandishi wa Habari kuwa rasmi ualianza Septemba 28 na yanatarajiwa kufungwa Septemba 30, 2023 na yanafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi International.

Amesema, “Maonesho haya ya msimu wa sita yamefana kutokana na wingi wa washiriki kuongezeka zaidi, lakini pia tumefurahi kuona kuwa Maonyesho yameleta mageuzi makubwa kwa Jamii kutokana na Wanawake Wajasiriamali kupata mafunzo maalumu ya namna ya kupata mitaji na kuendesha Biashara.”

Aidha, Maonesho hayo yanaenda sambamba na mafunzo maalumu ya Ujasiriamali kwa washiriki, yakijumuisha michezo na Utamaduni wa vyakula, huku Makau akiwataka Wanawake kuchangamkia fursa hiyo, ili kukuza Biashara zao.

Eddie Howe ampiga kijembe Pep Guardiola
Robertinho, Gamondi waanika mipango yao