Ligi ya Saudi Pro League inaripotiwa kutaka kuajiri baadhi ya waamuzi wakubwa barani Ulaya.

Klabu za Saudia zilitumia zaidi ya Pauni 800 milioni kununua wachezaji katika kipindi cha usajili wa dirisha la kiangazi ili kuongeza hadhi ya ligi hiyo.

N’Golo Kante, Jordan Henderson, Roberto Firmino na Riyad Mahrez ni baadhi tu ya mastaa wa walioikimbia Ligi Kuu England na kujiunga na Saudi Pro League.

Wakati huo huo, Neymar, Karim Benzema na Sergej Milinkovic Savic pia walihamia pande hizo na tayari wameshaanza kuzoea utamaduni wa Kiarabu.

Hata hivyo, gazeti la Times linadai kuwa Ligi ya Saudi sasa imedhamiria kuajiri baadhi ya waamuzi wakubwa wa Ulaya kwa muda wote.

Pia baadhi ya viongozi wa Ligi Kuu ya England wamezingatiwa huku mashabiki wakifurahia mchakato huo unaopangwa na waarabu.

Waamuzi kutoka Ligi Kuu England na Ulaya kwa ujumla wamejadiliwa kama wangependa kufanya mabadiliko kwenye taaluma zao kwa kuhamia Saudi.

Waamuzi wa kimataifa wamekuwa wakitumiwa na Ligi ya Saudi Pro League kwenye mechi maalumu kipindi cha nyuma, lakini sasa mabosi wanataka kuwapa mikataba ya kudumu kwenda kupiga kazi katika ligi hiyo.

Wazalishaji Vyakula vya Mifugo waitwa Maabara TVLA
Bakari Mwamnnyeto afichua siri za kambi