Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko mara baada ya kuwasha umeme katika Shule ya Sekondari Rusumo B, kupitia mradi wa REA III, mzunguko wa Pili Wilayani Ngara Mkoani Kagera, pia ameipatia kompyuta 10.

Dkt. Biteko ametoa kompyuta hizo hii leo Septemba 29, 2023 wakati wa hafla ya kuwasha umeme shuleni hapo na kuwataka Wanafunzi hao kuwa na nidhamu na juhudi katika masomo yao, ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Amesema, “tuanzishe madarasa ya kompyuta, tutawatafutia Kompyuta 10 kwa ajili ya wanafunzi wetu, tunafanya kila kinachowezekana msiishi maisha tuliyoishi.”

Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Rusumo B, Geze John alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha shule hiyo kupata umeme, hivyo kuondokana na changamoto ya umeme wa Sola iliyokuwa ikitumika.

Amesema, umeme huo wa Sola ulikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoa mwanga hafifu ambao ulikuwa unahatarisha uoni wa wanafunzi na kutotumika kwa muda mrefu, hivyo Wanafunzi kusoma kwa muda mfupi wakati wa usiku huku akishukuru kwa kupata Kompyuta hizo.

@Kwa hisani ya Lilian Lundo na Veronica Simba.

Umeme: Waziri Kapinga aipa TANESCO saa sita
Kocha Al Merreikh atamba kupindua matokeo