Klabu ya Chelsea iko tayari kusikiliza ofa kwa mlinzi wake kutoka Hispania, Marc Cucurella kuelekea dirisha dogo la usajili la Januari 2024, kwa mujibu wa ESPN.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 62 kutoka Brighton alicheza mechi yake ya pili msimu huu katika ushindi wa bao 1-0 wa raundi ya nne ya Kombe la Carabao dhidi ya klabu yake ya zamani, lakini bado hajacheza dakika hata moja kwenye Ligi Kuu ya England tangu Mauricio Pochettino awe kocha mkuu.

Cucurella aliiambia ESPN katika mahojiano yake ya Julai, alitaka kubakia kwenye klabu hiyo na kupigania nafasi yake, lakini ukosefu wa dakika za kucheza katika miezi ijayo kutamlazimisha afikirie vinginevyo.

Chelsea ilikuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ajiunge na Manchester United kwa mkopo msimu huu wa joto, lakini mpango huo ulishindikana baada ya Cucurella kucheza mechi ya awali ya klabu hiyo ya Kombe la Carabao dhidi ya AFC Wimbledon.

Kanuni za FIFA zinaeleza mchezaji hawezi kuwakilisha klabu tatu kwa msimu mmoja na hivyo mazungumzo hayo yalivunjika.

Ripoti kutoka Hispania zimehusisha na Real Madrid na uwezekano wa kuwasilisha ombi la mkopo Januari 2024 na matarajio ya kurejea katika nchi aliyozaliwa yanafikiriwa na Cucurella.

Mashabiki Arsenal wamkataa Kai Havertz
Azam FC kucheza bila Prince Dube Dodoma