Scolastica Msewa – Mafia.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amempa rungu Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge kunyang’anya Visiwa na viwanja uwekezaji wa Utalii Wilayani Mafia vilivyong’ang’aniwa na wawekezaji miaka mingi bila kuendelezwa kwa kutofanya chochote ili vigawiwe kwa wawekezaji wengine.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akifunga siku tatu za maonyesho ya uwekezaji wa katika uchumi wa buluu na kutangaza Utalii wa mazao ya Bahari katika kisiwa cha Mafia mkoani Pwani huku akisisitiza kuwa uwekezaji katika viwanja ni miezi 36 na endapo mtu hajaendeleza anatakiwa nyang’anywe, ili apewe mtu mwingine.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.

Amesema, “hatua hizo zifanyike kwa kuzingatia taratibu na Sheria za nchi kwani muda wa mwekezaji kumiliki eneo la uwekezaji bila kuendeleza ni miezi 36. Kweli ninyi mnawaacha tu? Sheria si zipo? Watu wa ardhi simpo. Wakuu wa Wilaya wengine mwende mkaainishe maeneo ya fulsa za uwekezaji wa Utalii mliyonayo yaliyoshikiriwa na wawekezaji kwa miaka mingi hayana kazi yoyote wala bila kuendelezwa.”

Aidha Waziri Mkuu pia amememtaka Mkuu huyo wa Mkoa kunyang’anya na kumpa uwekezaji mtu mwingine maeneo kisiwa ambayo yanamilikiwa bila kuendelezwa na kuongeza kuwa, “tunatangaza fulsa, tunaita Watalii, tunaita wawekezaji halafu Kuna mtu anamiliki bila kuendeleza nyang’anya tukabidhi wengine wawekeze hayo ndio maelekezo yangu.”

Teuzi 21 za Papa: Rais Samia ampongeza Kadinali Rugambwa
Umeme wawakutanisha Mawaziri Tanzania, Rwanda na Burundi