Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – CCM Taifa, iliyokutana katika kikao cmaalum hii leo Oktoba 1, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake – UWT na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi -UVCCM na imemteua Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT.

Kabla ya uteuzi huo, Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mkoani Tanga ambapo pia Kamati Kuu imemteua Fakii Raphael Lulandala, kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, kabla ya uteuzi huo, alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe.

Aidha, Kamati Kuu pia imemteua Ndugu Hamad Khamis Hamad, kuwa mgombea wa CCM wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Matembwe huku ikiwashukuru na kuwapongeza wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Mbarali, kwa kumchagua mgombea wa CCM, Bahati Kenneth Ndingo kuwa Mbunge wao katika
uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 20, 2023.

Kamati Kuu pia imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na ziara aliyoifanya katika Mikoa ya Lindi na Mtwara, ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa ambapo pamoja na mambo mengine, Rais alikagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za Wananchi.

Vilevile, Kamati Kuu hiyo pia impongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa namna anavyoiongoza Serikali katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi – CCM.

Hamasisheni zoezi usalimishaji silaha haramu - ACP Mlay
Teuzi 21 za Papa: Rais Samia ampongeza Kadinali Rugambwa