Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Viongozi wa dini kuwahimiza Vijana kufanya kazi kwa staha, weledi na uadilifu, ili kuzitumia rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo.

Majaliwa ametoa wito huo wakati wa Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilishaji katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea, kwenye kilima cha Peramiho, Songea mkoani Ruvuma.

Amesema, “Nchi yetu imebarikiwa fursa nyingi za kiuchumi, ili jamii ione matunda ya uwepo wa fursa hizo tunategemea sana nguvu kazi ya vijana katika kuzitumia rasilimali zilizopo. Tumieni nafasi zenu kuongeza msukumo wa malezi kwa vijana kwa kuweka mifumo ya kuwafuatilia kwa karibu.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, katika Hatua nyingine, Waziri Mkuu ameyapongeza madhehebu ya dini kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye sekta za elimu, afya, maji na huduma nyingine za kijamii hasa katika maeneo ya pembezoni.

Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Damian Dallu ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa katika shughuli mbalimbali za huduma za jamii na uinjilishaji zinazofanywa na kanisa katoliki nchini.

Amani, maendeleo: Serikali inathamini mchango wa Taasisi za Kidini
Makampuni binafsi yatakiwa kutoajiri Askari wazee