Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amempa Mkandarasi saa moja kutoa viatu vipya na vifaa vya usalama kwa mafundi wote katika ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko jijini Dodoma.
Agizo hilo limetolewa na wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Km 112.3) na kutoridhishwa na uchukuaji hatua za usalama kazini kwa wafanyakazi.
Aidha, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, kuhakikisha anasimamia usalama na afya za wafanyakazi mahali pa kazi katika maeneo yote ya miradi inayotekelezwa na wakala huo.
Amesema, “kuwataka kutoa vifaa vya usalama ikiwemo kofia ngumu, viatu, gloves, reflector na barakoa za kuzuia vumbi.”