Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema sababu kubwa ya timu hiyo kushindwa kutamba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ni kutokana na wachezaji wa kikosi hicho kupoteza umakini mwishoni.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Ijumaa (Septemba 29) Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku JKT ikitangulia kupitia kwa Daniel Lyanga kisha Gasper Mwaipasi kusawazisha mwishoni kabisa.

Malale amesema walistahili kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo ila kitendo cha kukosa umakini na nidhamu kubwa kwenye uzuiaji ndio sababu iliyowafanya kusawazishiwa kirahisi bao hilo.

“Baada ya kupata bao dakika zile za jioni wachezaji waliamini tayari mchezo umeisha hivyo kupoteza umakini kwenye uzuiaji na kuruhusu wapinzani wetu kusawazisha, tunarudi uwanja wa mazoezi kulifanyia kazi,” amesema.

Malale ameongeza licha ya kutowapa furaha mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuwapatia sapoti ila amewataka waendelee kuisapoti timu hiyo kwani makosa waliyofanya watayarekebisha kabla ya kucheza na Mashujaa, Oktoba 3.

Mchezo huo ni wa nne kwenye Ligi Kuu Bara kwa JKT msimu huu baada ya kuanza na ushindi wa l-0 dhidi ya Namungo kisha ikachapwa mechi mbili mfululizo ikilla 5-0 kutoka kwa Young Africans, halafu 2-l mbele ya KMC zote ikiwa ugenini.

FIGC kufikisha mahakamani Roberto Mancini
Lautaro Martinez atikisa kibiriti Inter Milan