Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria, Jose Peseiro amesema tena kwa msisitizo kwamba Mshambuliaji wa SSC Napoli, Victor Osimhen uwezo wake ni mkubwa na anaweza kupata namba ya kucheza kwenye klabu yoyote ile duniani.

Peseiro alifika mbali na kusema Osimhen ubora wake ni mkubwa na anaweza kushinda Ballon dOr kama ataweka malengo hayo.

“Yeye ni staa, ana uwezo wa kufunga mabao, kupambana na kukaba. Ni mchezaji mwenye nguvu sana anapokwenda kushambulia. Mabeki wanakuwa kwenye presha kubwa muda wote. Ana kasi, nguvu na anafunga mabao. Ni kama kichaa kwenye kufunga mabao,” alisema.

“SSC Napoli ni timu yenye nguvu. Ni mabingwa wa Italia. Anacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Ishu yake ya kuuzwa haijafanikiwa kwa sababu bosi wa SSC Napoli Aurelio De Laurentiis ana misimamo migumu. Sote tunafahamu, Osimhen amewaweka SSC Napoli mahali ambako wapo kwa sasa.”

Mifumo ya TEHAMA kufungwa Bohari kuu ya Jeshi
Wahasibu, Wakaguzi watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu