Inaelezwa kuwa Klabu ya Manchester United imeweka mezani majina matatu ya mabeki wa kati ikipiga hesabu kunasa huduma ya mmoja wao baada ya kuwa na wasiwasi kwamba Lisandro Martinez atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Man United imepanga kuingia sokoni kwenye dirisha la Januari 2024 mara tu litakapofunguliwa ili kunasa saini ya beki wa kati.

Kwenye orodha hiyo ya mabeki inaowataka yumo yule wa Bayer Leverkusen, Edmond Tapsoba, Antonio Silva wa Benfica na Jean-Clair Todibo wa Nice.

Martinez ameumia na kwamba majeruhi aliyopata yatamfanya kuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kitu ambacho kitamfanya kocha Erik ten Hag kuwa na upungufu wa watu kwenye safu yake ya ulinzi.

Jonny Evans alianzishwa kwenye mechi dhidi ya Burnley, lakini hilo halikuwa na namna kwa sababu Ten Hag hakuwa na chaguo jingine.

Raphael Varane hakuwa fiti kucheza mechi, hivyo alianzia benchi huko Harry Maguire na Luke Shaw nao walikuwa majeruhi.

Na sasa gwiji wa masuala ya usajili, abrizio Romano amesema kuna mabeki wa kati watatu Todibo, Tapsoba na Silva wanapigiwa hesabu na Man Utd ili saini zao zinaswe kwenye dirisha la Januari 2024.

Man United juzi Jumamosi (Septemba 30) ilikuwa na shughuli ya kuwakabili Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika uwanjani Old Trafford.

Kairuki ataka matumizi ya taaluma kuzisemea Taasisi
Serikali yaweka mikakati kupunguza tatizo la umeme