Vikundi vya Ulinzi Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, vimetakiwa kufanya kazi ya kuzuia na kutatua changamoto za usalama katika jamii na sio kushirikiana na wahalifu kutenda uhalifu

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Babati, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Mayala Ngollo hii leo Octoba 2, 2023 wakati wa kukabidhi vitendea kazi kwa Kikundi cha Ulinzi Kata ya Maisaka ‘B’ ofisini kwake.

Akipokea vitendea kazi hivyo, Kiongozi wa Kikindi hicho Bernard Raphael amelipongeza Jeshi la Polisi Wilayani humo na kuitaka jamii kutoa ushirikiano pindi wanapoona uhalifu na mhalifu.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Babati, limeendelea kushirikiana na Vikundi hivyo kwa kuwapatia vitendea kazi mbalimbali, ikiwemo filimbi na nguo zenye kuakisi mwanga.

Wahasibu, Wakaguzi watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu
Lisandro Martínez aongeza machungu Man Utd