Serikali imewataka Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa misingi ya uadilifu na uaminifu wa hali ya juu ili kuongeza tija na ufanisi katika maendeleo ya nchi.

Akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya amesema NBAA inatakiwa kuisaidia serikali na kuhakikisha kanuni na miongozo ya uadilifu inafuatwa na wanachama wake wote ili atakaenda kinyume hatua kali zichukuliwe dhidi yake na iwe fundisho kwa wengine.

Amesema, Halmashauri zote nchini ziwatumie wataalamu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ili kupunguza migogoro ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inawakabili wananchi katika kutekeleza miradi hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu amewataka wahitimu wote kuhakikisha wanasoma taratibu za NBAA ili waweza kujua ni namna gani ya kwenda kufungua ferm ya mahesabu na sio kwenda kusaini mahesabu.

Aidha, ametoa rai kwa wazazi, walenzi na wajaajiri wa Sekta za umma na binafsi kuendelea kuwasapoti vijana na watumishi wao ili waweze kufanya mitihani ya bodi na kufuzu kwa uwekezaji wa taaluma ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ni uwekezaji unaolipa.

Victor Osimhen atabiriwa Ballon dOr
Vikundi vya Ulinzi vyaaswa kutoshiriki uhalifu