Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki leo amekutana na Kamati ya kitaifa ya Maandalizi ya Onesho la Kimataifa la Swahili International Tourism Expo na kukagua maandalizi yake yatakayoanza Oktoba 6 hadi 8, 2023 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho ambapo Kairuki amewataka wahusika kuzingatia taaluma ili kuzielezea Taasisi zao kwa ufasaha na kuwa na utaratibu wa kujiendeleza kupitia fursa za mafunzo kwa njia ya mtandao.

“Amesema, “tutumie vizuri mafunzo kwa njia ya mtandao yanayohusu masuala ya utalii katika kujiendeleza na kujifunza zaidi, ili kuijua zaidi sekta hii.”

Onesho hilo, litahudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika wakiwemo wanunuzi wa bidhaa za utalii ambao hutembelea maonesho ya Utalii kwa lengo la kujenga ushirikiano wa kibiashara na wafanyabiashara.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa Wakurugenzi na baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania, TANAPA, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro – NCAA na wadau kutoka Sekta Binafsi.

Waliogundua chanjo ya Uviko-19 Washinda Tuzo ya Nobel
Watatu wanawindwa Old Trafford