Klabu ya Arsenal imepanga kumgeukia kiungo wa Manchester City na England, Kalvin Phillips katika dirisha lijalo ikiwa ni katika harakati za kuboresha eneo hilo.

Phillips ambaye amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man City, anaonekana kuwa mbadala sahihi wa Thomas Partey ambaye amekuwa akitajwa kwamba yupo kwenye hatihati kuondoka ifikapo dirisha la majira baridi na mwisho wa msimu.

Tangu kuanza kwa msimu huu Phillips amecheza mechi tano za michuano yote na mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028.

Ikiwa Arsenal itashindwa kumsajili moja kwa moja imepanga kuomba kumchukua kwa mkopo ambaye naye anaonekana kutamani kuondoka ili kujiunga na timu itakayompa nafasi kubwa ya kucheza.

Kocha Mikel Arteta anataka kumuondoa Partey kwa sababu amekuwwa akisumbuliwa sana na majeraha yanayosababisha akae nje ya Uwanja muda mrefu.

Rostam Aziz aikana Young Africans
Simba SC yaomba mchezo kusogezwa mbele