Mfanyabiashara wa kimataifa, Rostam Aziz amekanusha taarifa za mtandaoni zinazodai kuwa anataka kuwekeza katika Klabu ya Soka ya Young Africans kwa kiasi cha Sh Bilioni 30.

Kwa mujibu wa taarifa ya matapeli hao, Rostam ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Taifa (Taifa Group Ltd) anadaiwa kukutana na Young Africans na kufikia makubaliano ya yeye kuwekeza kiasi hicho cha fedha kama sehemu ya asilimia 49 ya hisa ya klabu hiyo.

Mbali na hilo, matapeli hao wa mtandaoni walikwenda mbele zaidi na kueleza kwamba, Rostam alikuwa amefikia makubaliano na Young Africans kwa kuutaka uongozi wa klabu hiyo kutafuta wawekezaji wengine wawili zaidi ambao nao wangetoa kiasi cha Sh bilioni 20 kwa pamoja ili kukamilisha nakisi ya hisa asilimia 49.

Rostam amekanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa hajawahi kukutana na viongozi wa Young Africans hivi karibuni, kwani yupo nje ya nchi kwa muda mrefu kwa shughuli zake za kifamilia.

AFCON 2027: Waziri Kenya azikumbusha Tanzania, Uganda
Kalvin Phillips kumbadili Partey