Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Man Utd Zlatan Ibrahimovic ana wasiwasi na Kocha Mkuu wa kikosi cha klabu hiyo Erik ten Hag hana uzoefu wa kudili na wachezaji wakubwa.

Kocha wa Mashetani Wekundu, Ten Hag tangu atue kikosini hapo msimu uliopita ameachana na wachezaji wawili wakubwa Cistiano Ronaldo, David De Gea huku sasa akiwa na mgogoro na Jadon Sancho.

Zlatan, ambaye ana sifa kubwa katika mchezo huo, amesema: “Kutoka Ajax kuja United kama alivyofanya ni tofauti kubwa nimekuvwa katika klabu zote mbili.

“Kuna aina tofauti ya nidhamu. Ajax ni klabu yenye vipaji. Wana vipaji bora katika klabu. Hawana nyota wakubwa. Je, uzoefu wa kocha huyu ni nini? Vijana wenye vipaji, anakuja United, ni mawazo tofauti.

“Wachezaji waliopo wanatakiwa kuwa nyota wakubwa. Sidhani kama unatoa huduma sawa.

“Unampa kocha muda gani, inategemea na wamiliki wanataka nini, lakini ukiwasikiliza mashabiki, huna muda mwingi kwa sababu wanataka kushinda, nawaelewa kwa sababu wapo wamezoea kushinda na wanataka bado kushinda.”

United wameanza vibaya msimu wao wa ligi kuu katika kipindi cha miaka 34.

Maagizo ya Waziri Mkuu kwa TAKUKURU, Polisi
Azim Dewji: Tumechoshwa na Robo Fainali Afrika