Ratiba rasmi ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho itapangwa kesho ljumaa (Oktoba 06) jijini Johanesburg, Afrika Kusini, ambapo timu za Tanzania zitajua wapinzani wao.
Young Africans na Simba SC ndio klabu pekee za Tanzania baada ya Singida Fountain Gate kuondolewa na Future FC ya Misri Jumapili (Oktoba Mosi) kwa jumla ya mabao 5-2.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Singida Fountain Gate ilishinda kwa bao 1-0 kabla ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 katika mchezo wa marudiano nchiní Misri, Jumapili iliyopita.
“Ratiba rasmi ya hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Shirikisho Afrika itafanyika Johannesburg, Afrika Kusini lịumaa Oktoba 6, 2023 kuanzia saa 7:00 mchana sawa na saa 8:00 mchana kwa saa za Tanzania,” imesema taarifa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.
Droo hiyo itaanza na upangaji wa ile ya Kombe la Shirikisho na baadae kufuatiwa na ile ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Kufuatia raundi za awali zilizoanza mwezi Agosti, jumla ya klabu 16 zilifuzu kwa hatua hiyo ya makundi.
Mabingwa wa mashindano hayo mawili wote wamepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi, Al Ahly (Ligi ya Mabingwa) na USM Alger (Kombe la Shirikisho) watakuwepo katika ratiba pamoja na timu zingine wakisaka ufalme wa msimu huu.
Miongoni mwa timu zilizomo katika Ligi ya Mabingwa ni pamoja na timu ya Mauritania ya FC Nouadhibou ambayo ilifanya maajabu kwa kuitoa Real Bamako wakati Jwaneng Galaxy ya Botswana waliwatoa mabingwa wa mwaka 1995, Orlando Pirates.
Timu zote zilizofuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ni pamoja na Al Ahly (Misri) Al Hilal (Sudan), Asec Mimosas (lvory Coast), CR Belouizdad (Algeria), ES Sahel (Tunisia), Esperance (Tunisia), FC Nouadhibou (Mauritania), Jwaneng Galaxy (Botswana) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini).