Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefika kata Murusagamba iliyopo Wilayani Ngara Mkoani Kagera kufatia agizo alilopewa na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko la kuleta suluhisho la upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.

Aweso amesema, Wizara ya Maji imetoa shilingi milioni 250 kwaajili ya kuanza kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Murusagamba na kumtaka mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi, kutumia wafungwa kuchimba mitaro ili ndani ya siku 30 mradi huo uwe umekamilika na kukabidhiwa kwa wananchi.

Kutokana na watu kuongezeka katika kijiji cha Murusagamba Aweso amesema kumepelekea huduma ya maji kuwa hafifu hivyo mradi huo unakwenda kupanuliwa na kuwekewa miundombinu mipya hili maji yawafikie wananchi kwa urahisi.

Aidha, amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Kagera kutangaza mradi wa maji wa kijiji cha Ntanga wenye gharama Zaidi ya shilingi milioni 700 ili wananchi wa kijiji hicho waanze kunufaika na maji.

Sambamba na hayo ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Kumubuga kufika ofisi za mkuu wa Wilaya kutoa maelezo ya lini anamaliza mradi anaoujenga kutokana na kuchelewa kwa mradi huo.

Vijana wapaze sauti athari mabadiliko Tabianchi - Dkt. Jafo
UTPC yazindua mpango Mkakati 2023-2025