Imefahamika kuwa, winga wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Leroy Sané yuko kwenye mipango ya usajili wa Mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona.

Sane ambaye amekuwa akifanya vizuri kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Bundesliga, pia anahusishwa kutakiwa na Real Madrid ambao wanafuatilia mkataba wake unaomalizika mwaka 2025.

Winga huyo msimu huu amefanikiwa kufunga mabao sita katika mechi nane, Bayern wanaweza kumuuza ikiwa hataongeza mkataba kama inavyotarajiwa.

Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez, alitaka kusajili winga wa kushoto na chaguo lake lilikuwa kwa Sané, lakini klabu haikuwa na fedha za kufanya hivyo.

Baada ya kuondoka kwa Dembélé, inaonekana Raphinha ndiye atapewa nafasi kubwa kikosini hapo, lakini bado Barcelona inaendelea kuwa na uhitaji wa Sané.

GGML washusha Basi jipya la Geita Gold FC
Lionel Messi kurudishwa FC Barcelona