Aliyekuwa Beki wa Inter Milan, Marco Materazzi, amebainisha kwamba, anataka kufahamu kwa nini Romelu Lukaku hakurejea klabuni hapo na kuamua kwenda AS Roma kwa mkopo akitokea Chelsea.

Materazzi amebainisha kwamba, Lukaku msimu uliopita alifanya mazungumzo ya kujiunga na Juventus wakati akiwa bado ni mchezaji wa Inter Milan, kitu ambacho ni kama usaliti.

“Ni aibu. Nataka kufahamu nia yake ilikuwa nini,” alisema Materazzi.

Alipoulizwa ni vipi atakaribishwa Inter katika mchezo wa Serie A utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu huko San Siro, Materazzi alisema: “Anafahamu, nadhani itakuwa vibaya. Ni kawaida kwamba alisaliti mara moja, akasamehewa, kisha akasaliti mara ya pili.”

Lukaku amewahi kuitumikia Inter Milan vipindi viwili tofauti, awali ilikuwa 2019 hadi 2021 alipotua mara ya kwanza akitokea Manchester United, kisha msimu wa 2022-2023 akicheza kwa mkopo akitokea Chelsea.

Chongolo kuteta na Bashe mradi Skimu ya umwagiliaji
Ben Chilwell hadi Desemba 2023