Mwamuzi Darren England hatarajiwi kuchezesha mechi nyingine za Liverpool msimu huu kufuatia makosa ya VAR yaliyotokea katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Hotspur mwishoni mwa juma lililopita.

England mwenye umri wa miaka 37, alihusika aliposhindwa kubadili uamuzi baada ya Luis Diaz kufunga bao halali hata hivyo likakataliwa kwa madai ya kuotea, Liverpool ikilala 2-1.

Mstari ulichorwa ukionyesha Diaz akiwa sehemu sahihi baada ya kudhaniwa kuwa aliotea, lakini mwamuzi huyo na msaidizi wake Dan Cook hawakufahamu walitakiwa kubadili uamuzi.

Mechi iliendelea na wasimamizi wa VAR hawakuingilia kati kutoa uamuzi, hiyo ikimaanisha kwamba bao la Diaz lilikataliwa.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp aliomba mechi kurudiwa lakini taarifa zimethibitishwa kwamba mwamuzi huyo hatapangwa katika mechi zote za Liverpool msimu huu.

Hata hivyo, inaaminika kwamba mwamuzi huyo alipewa sapoti na kiongozi wa waamuzi (PGMOL), Howard Webb na hatafukuzwa kazi kama ilivyodhaniwa.

Majaliwa aagiza Kampuni za upimaji viwanja zichukuliwe hatua
Huu hapa makakati wa Robertinho Simba SC