Uongozi wa Singida Fountain Gate wa klabu hiyo bado unaendelea na mpango wa kusaka kocha mpya atakayekinoa kikosi cha klabu hiyo, huku wanaoatajwa hadi sasa ni makocha Pablo Franco na Didier Gomes waliowahi kuinoa Simba SC kwa vipindi tofauti.

Singida FG inayonolewa na kaimu kocha mkuu, Ramadhan Nswanzurimo kwa sasa imekuwa haina kocha mkuu baada ya Mjerumnani, Ernst Middendorp kutimka Septemba 19, mwaka huu ikiwa ni muda mchache tangu ajiunge na timu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, mazungumzo baina ya viongozi wa Singida FG na makocha hao yanaendelea na kama mambo yataenda sawa basi mmoja kati yao atapewa mikoba ya kukiongoza kikosi hicho.

“Ni kweli tumekuwa kwenye mazungumzo na makocha mbalimbali lakini bado hatujafikia makubaliano yoyote, sisi kama viongozi hatutafanya maamuzi ya haraka kwa sababu ya kile kilichotokea mwanzo,” kimesema chanzo cha habari kutonga Singida FG.

Kwa upande wa Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Ibrahim Mirambo akizungumzia juu ya makocha hao, amesema amekuwa akisikia tu kuhusu taarifa hizo ila wao kama viongozi bado wana imani na benchi lilolopo sasa.

“Sijajua hizo taarifa zinatoka wapi ila ninachojua mimi tuna benchi bora la ufundi ambalo linaweza kuongoza timu hadi pale tutakapoamua vinginevyo, nisingependa kuzungumzia sana kuhusu tetesi za mitandaoni,” amesema.

Pablo Franco

Hata hivyo, Nswanzurimo ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi, viongozi wangetamani kuendelea kumuona akiifundisha timu hiyo hadi mwisho wa msimu, ingawa itategemea na kiwango ambacho timu hiyo itaonyesha katika michezo mbalimbali.

Timu hiyo ilianza msimu na Mholanzi, Hans Van de Pluijm aliyeiwezesha kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika huku akiiongoza katika mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu Bara na Tànzania Prisons ulioisha 0-0, Agosti 22, mwaka huu.

Pacome Zouzoua: Kipigo kimetupa umakini
Ntibanzokiza awashtua wachezaji Simba SC