Baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na uzi wa Real Madrid kwenye mashindano yote ndani ya muda mfupi, magwiji wa soka Barani Ulaya wameanza kumchambua Jude Bellingham na kusema ana ufundi mwingi kama Zinedine Zidane na Di Stefano.

Bellingham mwenye umri wa miaka 20 raia wa England, amekuwa gumzo Barani Ulaya na Hispania nzima kwenye magazeti, TV, redio na mitandao ya kijamii.

Mechi tisa, mabao nane na sasa wachambuzi wengi wanamuita Di Stefano mdogo, Zidane mdogo na Ilikuwa hivyo kwenye vichwa viwili vya habari baada ya kufunga bao safi kwenye UEFA dhidi ya SSC Napoli ya Italia.

Alpoulizwa kuhusu ulinganisho wake na nyota hao wa zamani wa Madrid Bellingham alisema: “Ndoto yangu ilikuwa siku zote kuwa sehemu ya La Liga katika kiwango kikubwa zaidi na naamini nitafika kwenye kiwango hicho.”

Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti alisema: “Ninashangaa ana umri wa miaka 20 tu lakini anaonekana kama ana miaka 30 kwa sababu ya tabia na mtazamo wake.”

“Sio kawaida kwa kijana wa miaka 20. Ana ubora mkubwa, nguvu za kimwili na ujuzi. Ananishangaza kama anavyofanya kwa kila mtu.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 7, 2023
Pacome Zouzoua: Kipigo kimetupa umakini