Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani humo msimu huu 2023/24, huku mchaka mchaka kwa timu shiriki katika hatua hiyo ukitarajiwa kuanza Novemba 24.

CAF imepanga makundi hayo mjini Johannesburg-Afrika Kusini leo Ijumaa (Oktoba 06), chini na Mkuu wa Idara ya Mashindano ya Shirikisho hilo, Khalid Nassar.

Mabingwa wa Tanzania Bara Young Africans ambao watashiriki hatua hiyo baada ya miaka 25 kupita, wamepangwa Kundi D, huku ndugu zao Simba SC ikiangukia Kundi B.

Bingwa wa michauno hiyo msimu wa 2022/23 Al Ahly kutoka Misri amepangwa Kundi D.

Kundi A:  FC Nouadhibou, TP Mazembe, Mamelodi Sundowns na Pyramids

Kundi B:  Simba,  ASEC Mimosas, Jwaneng Galaxy na Wydad AC

Kundi C: Espérance de Tunis, Étoile du Sahel,   Petro de Luanda na Al Hilal

Kundi D:  CR Belouizdad  Al Ahly, Young Africans na Medeama

Charles Ilanfya afichua siri ya kumfunga Diara
Luis Enrique: Ninastahili kulaumiwa