Huenda Mabingwa wa Soka nchini Hispania FC Barcelona wakapambana na wapinzani wao wakuu kwenye Real Madrid kwenye mechi ya EI Clasico bila ya Mshambuliaji wao hatari kutoka nchini Poland, Robert Lewandowski.

Lewandowski anatazamiwa kulikosa pambano hilo ambalo litapigwa Oktoba 29, mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu ‘ENKA’ ambayo aliyapata hivi karibuni.

Taarifa kutoka kwenye timu ya madaktari wa timu hiyo ni kuwa Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kwa ajili ya kujiuguza majeraha hayo na ataikosa mechi hiyo ya El Clasico.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Lewandowski anasumbuliwa na majeraha hayo ya kifundo cha mguu wa kushoto na sasa madaktari wanaendelea kuangalia jeraha hilo.

Tisa wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji Njombe
Pep Guardiola atoa angalizo kwa mashabiki