Naibu Kamishina wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, Zainab Bungwa ameungana na Vijana zaidi ya 300 wa Mataifa 24 Ulimwenguni ambao kupanda jumla ya miti ya mikoko 1,000 katika Kunduchi na Mbweni jijini Dar es Salaam wakilenga kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Bungwa ambaye alimwakilisha Kamishina wa Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo amesema Vijana hao pia wameongozana na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Uongozi wa Vijana na Mabadiliko ya Tabianchi wa Kimataifa, Ejaj Ahmad.

Amesema, “tuungane na Watanzania wenzetu hasa vijana kupanda mikoko na kuweka mikakati ya kuhamasisha ushiriki wa Vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Na ndio maana leo hii tumepanda mikoko ambayo ni muhimu sana katika ulinzi wa pwani kwani Mikoko inaweza kunyonya hewa ukaa tani nne mpaka tani 10 zaidi ya misitu mingine.”

Vijana hao ni wale ambao walishiriki Kongamano la tatu la Kimataifa la Viongozi Vijana na Mabadiliko ya tabianchi (GLOBAL YOUTH CLIMATE SUMMIT) linalofanyika jijini Dar es Salaam ambapo waliitumia nafasi hiyo, kuileza dunia kuwa mikoko ikitunza inaweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Joash Onyango, Singida FG mambo safi
Uteuzi wa Messi wazua kizaazaa Marekani