Boniface Gideon – TANGA.

Wachezaji 25 wa Timu ya mpira wa miguu ‘Bomboka Fc ‘ inayoshiriki ligi ya Mkoa wa Tanga, wamekabidhiwa Bima za Afya, zilitolewa na Wafanyakazi wa Taasisi ya Gift of hope Foundation, chini ya Mwenyekiti wa Timu Said Bandawe.

Akikabidhi Bima hizo , Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Abdarahaman Shiloo aliwapongeza Viongozi wa Timu hiyo kwa hatua kubwa waliyoifikia kwa kuhakikisha wachezaji wa Timu hiyo wanakuwa na Bima za Afya.

Aidha, aliwataka Wanamichezo na Jamii kuweka utaratibu wa kukata Bima za Afya, ili kuwapa unafuu wa matibabu wanapopatwa na maradhi au ajari akisema, “Bima hii ni Bei nafuu, ukiwa na shilingi 30,000 unauwezo wakukata wewe na familia yako mkapata matibabu katika hospitali zote za umma nchini.”

Shiloo pia aliwataka Wadau mbalimbali hususani wa michezo kuhakikisha vikundi vyao vinakuwa na Bima za Afya, ili kuwapa unafuu Wanamichezo kupata huduma ya matibabu kwa wakati.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Timu hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Gift of hope Foundation inayotoa msaada kwa waraibu wa Dawa za kulevya, Said Bandawe alisema Bima hizo zimetolewa na Wafanyakazi wa Taasisi hiyo ikiwa ni Sehemu ya kuhakikisha usalama pale wanapopata majeraha uwanjani.

Rais Dkt. Samia awasili India
Mbunge Mulugo alala chini ili achafuke kama Wananchi wake