Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini New Delhi, India hii leo Oktoba 8,  2023 kwa ajili ya kuanza ziara ya Kitaifa ya siku nne nchini humo.

Mapokezi rasmi ya Rais Dkt. Samia yatafanyika Oktoba 9, 2023 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa India, Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi.

Ziara ya Rais Dkt. Samia nchini India ni mwendelezo wa ushirikiano na uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi  mbili ambapo sekta muhimu nchini kama Afya, teknolojia, kilimo, uchumi wa buluu, biashara, uwekezaji, maji na elimu zinatarajiwa kuwa kipaumbele wakati wa majadiliano.

Dkt. Biteko kushuhudia Sherehe za Uhuru Uganda
Bomboka FC wakabidhiwa Bima za Afya