Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini New Delhi, India hii leo Oktoba 8,  2023 kwa ajili ya kuanza ziara ya Kitaifa ya siku nne nchini humo.

Mapokezi rasmi ya Rais Dkt. Samia yatafanyika Oktoba 9, 2023 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa India, Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea na kazi wakati akiwa safarini kuelekea Mji wa New Delhi nchini India kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 08 Oktoba, 2023. Mhe. Rais Samia alitumia usafiri wa Ndege ya Shirika la ATCL ambalo limeanza safari zake kutoka Tanzania mpaka India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea na kazi wakati akiwa safarini kuelekea Mji wa New Delhi nchini India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India.
Rais Samia mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya Kitaifa Oktoba 8, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma cha asili ya India.
Rais Samia Suluhu Hassan akipiga makofi kufurahia kikundi cha ngoma cha asili ya India kikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma cha asili ya India kikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Watanzania mara baada ya kuwasili New Delhi nchini India kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya Kitaifa Oktoba 8, 2023.

Ziara ya Rais Dkt. Samia nchini India ni mwendelezo wa ushirikiano na uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi  mbili ambapo sekta muhimu nchini kama Afya, teknolojia, kilimo, uchumi wa buluu, biashara, uwekezaji, maji na elimu zinatarajiwa kuwa kipaumbele wakati wa majadiliano.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 9, 2023
Dkt. Biteko kushuhudia Sherehe za Uhuru Uganda