Serikali ya Israel, imetangaza rasmi kuingia vitani dhidi ya Wanamgambo wa Hamas huko Gaza na kuweka mazingira ya Jeshi la Israel kujibu shambulizi la kushtukiza la Wanamgambo hao dhidi ya Taifa hilo la Kiyahudi.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema nchi yake tayari ipo vitani na Hamas, huku mashambulizi ya wanamgambo hao yakiendelea na kuingia siku ya nne hii leo, licha ya kuwa kauli yake hiyo hikuwa rasmi.

Kabla ya kura ya baraza la mawaziri, Netanyahu, alitangaza kwamba Israeli italipiza kisasi dhidi ya Hamas, licha ya wanajeshi wa Israeli kuanzisha mapambano na wapiganaji wa Hamas.

Mashambulizi hayo yalifanywa katika mitaa ya kusini mwa Israeli yakiwemo ya anga ya kulipiza kisasi ambayo yaliharibu majengo ya Gaza, ambapo zaidi ya watu 200 walifariki na wengine kutekwa wakiwemo Wanawake, Watoto na Wazee.

Gamondi: Ninaitaka Azam FC, CAF baadae
Urais DRC: Wagombea 23 kumkabili Tshisekedi