Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefamyiwa mapokezi ya kufana na mwenyeji wake Rais wa India, Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi, hii leo Oktoba 9, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa India, Droupadi Murmu (Kushoto), pamoja na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan), iliyopo New Delhi nchini humo hii leo Oktoba 9, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima wakati wa hafla ya mapokezi yake katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan), jijini New Delhi nchini humo Oktoba 9, 2023.
Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa kwenye mapokezi yake katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan), New Delhi nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi mara baada ya kuwasili katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari katika Jengo Maalum la kupokelea wageni wa Kitaifa Hyderabad House New Delhi Nchini India hii leo Oktoba 9, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali lililoulizwa na Waandishi kuhusu mategemeo ya ziara yake nchini India hii leo Oktoba 9, 2023.
Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi nchini India hii leo Oktoba 9, 2023.

Jose Mourinho anaitaka Saudi Arabia
Gamondi: Ninaitaka Azam FC, CAF baadae