Watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa wametakiwa kuwa wabunifu na wachukue hatua kulinda maadili ya Mtanzania, sambamba na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta furaha na ufanisi mahala pa kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wakati alipokutana na kufanya kikao na Watumishi hao katika ofisi za Wizara hiyo ziliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa na Watumishi kilichofanyika katika ofisi ya Wizara hiyo, iliyopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Amesema, “Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekua akitusisitiza tulinde maadili yetu na anapenda kutangaza Utamaduni wetu na ndiyo maana anaitwa Chifu Hangaya. Mhe. Rais kuwa Chifu ni fursa ya kuhakikisha tunaisimamia ajenda yetu ya kulinda na kutangaza Utamaduni wa Taifa letu.”

Aidha, Msigwa ameongeza kuwa Wizara kupitia Idara ya Utamaduni na Idara ya Sanaa ina wajibu wa kuwaelimisha Vijana ili wajue kuwa Tanzania ina Utamaduni na maadili yake, akiwataka wawe sehemu ya kulinda na kuendeleza maadili na Utamaduni wa Taifa.

Miradi uhifadhi, usimamizi Mazingira kuibuliwa katika jamii
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 10, 2023