Rais wa zamani wa Shiriksho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter, amekosoa uamuzi wa shirikisho hilo kubariki Fainali za Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa katika mataifa sita na mabara matatu.

Morocco, Hispania na Ureno zilitawazwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo ya mwaka 2030, huku Uruguay, Argentina na Paraguay pia zikiwa mwenyeji wa mechi za ufunguzi kuadhimisha miaka l00 ya michuano hiyo, FIFA ilisema katika taarifa yake Jumatano ya juma lililopita.

Uamuzi huo umekosolewa na Blatter, ambaye alikuwa Rais wa FIFA kuanzia mwaka 1998 hadi 2015, kabla ya kulazimika kutolewa baada ya madai ya rushwa.

“Ni upuzi kusambaratisha mashindano kwa njia hii” amesema Blatter akiliambia gazeti la Sonntags Blick la nchini Uswis.

“Fainali za Kombe la Dunia lazima ziwe tukio fupi,” amesema akiongeza hii ilikuwa muhimu kwa utambulisho wa hafla hiyo, kwa shirika na kwa wageni.

Blatter, ambaye zamani alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika kandanda, aliwahi kuikosoa FIFA kwa kuipa Qatar mashindano ya 2022, akisema nchi hiyo ya Mashariki ya Kati ni ndogo sana.

Blatter mwenye umri wa miaka 87, amesema mashindano ya mwaka 2030 yanapaswa kufanyika Amerika Kusini, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 ya tukio la kwanza ambalo liliandaliwa nchini Uruguay.

Gamondi akusanya mafaili Kundi D Afrika
Kocha Mtibwa Sugar ajitetea