Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa Mwanamke wa kwanza kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), toka Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha Nchini India.

Shahada hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India hii leo Oktoba 10, 2023.

Viongozi wwengine wawili pekee ndiyo ambao waliwahi kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Hayati Shinzo Abe.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit.
Rais Samia akiwa kwenye hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru.
Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa), aliyopatiwa Rais Samia hii leo Oktoba 10, 2023.

Mapigano Palestina: Miili 1,500 yapatikana
TAFIRI kutafiti taarifa sahihi rasilimali za uvuvi