Muda wa Jadon Sancho kuomba msamaha kwa kocha Erik ten Hag unaelekea kumalizika pale Manchester United na kwamba sasa ni wazi kuwa anaelekea mwisho katika viungo vya Old Trafford, kwa mujibu wa ESPN.

Sancho bado hajaomba msamaha baada ya kudai kuwa Ten Hag alidanganya hadharani kuhusu sababu za yeye kuachwa kabla ya kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Arsenal Septemba 03, mwaka huu.

Ten Hag alimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kuomba msamaha, lakini hadi sasa amekataa kufanya hivyo.

Ten Hag hajafunga kabisa mlango juu ya uwezekano wa Sancho kujumuishwa kwenye kikosi, lakini anatakiwa kwanza kuomba msamaha baada ya chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii.

Sancho amebakia kwenye programu ya mazoezi ya mtu binafsi katika kambi ya mazoezi ya United kule Carrington na ana mwingiliano mdogo na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza.

Jumamosi (Oktoba 07), alitazama timu ya vijana chini ya unri wa miaka 18 pale Carrington wakati timu ya kwanza iliwasili Old Trafford kabla ya ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford.

Sancho, ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 73 kutoka Borussia Dortmund mwaka 2021, yuko chini ya mkataba hadi mwaka 2026 na kuna wasiwasi katika klabu kuhusu hali ya kifedha ambayo inaweza kuwa muhimu ili kuwezesha kuondoka kwake.

Thamani yake sokoni imeshuka kwa kiasi kikubwa baada ya misimu miwili iliyokatisha tamaa pale United na klabu chache sana duniani zinaweza kufikia mshahara wake, ambao ni zaidi ya pauni 300, 000 kwa juma.

Chanzo kimoja kiliiambia ESPN kwamba wachezaji wenzake na Sancho wa England akiwano Harry Maguire, Marcus Rashford na Luke Shaw walimtaka Sancho kuomba msamaha ili kurejea kwenye timu, lakini bado hajafanya hivyo.

Kamati ya waamuzi yasisitiza haki Ligi Kuu
Pablo, Gomez ngoma ngumu Singida Fountain Gate