Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema maandalizi ya ibada ya Misa maalum ya kumbukizi ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere yamekamilika ambapo amewataka wananchi kushiriki katika Misa hiyo.

Sendiga ameyasema hayo hii leo Oktoba 11, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Uwanja wa Kwaraa mjini Babati na kuongeza kuwa, ibada hiyo itaanza majira ya saa moja na nusu asubuhi Oktoba 14, 2023 katika Kanisa katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga.

Amesema, ibada hiyo itahudhuriwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Viongozi mbalimbali toka Tanzania Bara na Zanzibar.

Aidha, Sendiga pia amewataka wananchi kushiriki katika kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru, ambapo sherehe hizo pia zitafanyika katika Uwanja huo wa Kwaraa na kusema tayari wageni mbal;imbali wameshawasili.

Guardiola akataa kuzungumzia ugomvi Emirates
Serikali kushughulikia changamoto ya Umeme