Mabadiliko Mfumo wa elimu yanaweza kuchangia kumaliza au kupunguza rushwa ya ngono ambayo husababisha matatizo kwa wasichana na kuathiri maendeleo na haki zao hususani wale walio katika vyuo vya elimu ya juu.
Hayo yamebainishwa wakati maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka, huku baadhi ya Wanafunzi wakike wanaosoma katika vyuo vikuu nchini Tanzania walitoa wito kwa Serikali kufanya mabadiliko katika mfumo wa elimu, ili kumlinda mtoto wa kike dhidi ya rushwa ya ngono.
Wanafunzi hao, wamesema mfumo uliopo unaonekana kutoa mianya ya rushwa kwa walimu wa wasichana hao na kusema sheria zilizopo huwalinda walimu mara inapogundulika uwepo wa suala la rushwa na kwamba jamii, impatia mtoto wa kike elimu na kutatua changamoto zinazowakabili wakati wa kutafuta elimu.
Kwa upande wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Bahari – DMI cha jijini Dar es Salaam, Happyness Mkomimikinda amesema mfumo uliopo unampa Mwalimu uwezo wa kumbana mwanafunzi anaposhindwa kufaulu masomo yake huku Makamu wa Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT Dorice Alchard akisema Serikali iangalie uhuru uliowapa Wanachuo kwani wengi wao huutumia vibaya kwa kuvaa mavazi yasiyo na maadilili.