Klabu ya Simba leo Alhamis (Oktoba 12) imezindua jezi mpya maalum kwa ajili ya mashindano ya African Football League ‘AFA’ yatakayozinduliwa rasmi jijini Dar es salaam baadae mwezi huu.

Simba SC itacheza dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Benjamin Mkapa Ijumaa (Oktoba 20).

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally amesema, wanakwenda kuzitumia jezi hizo kwenye michuano ya African Football League ambayo ni mashindano yao pekee yao!

“Unapokwenda kwenye sikukuu ni sunna kuvaa nguo mpya, kwa hiyo Sunderland The Only One akaona tunapokwenda kwenye sikukuu ya Oktoba 20 wanasimba tusivae jezi za zamani badala yake tuvae jezi mpya zinazolingana na hadhi ya mashindano hayo.” Amesema Ahmed Ally

Ukarabati Uwanja wa Mkapa bado kidogo tu!
Mifumo ya Matibabu Vituo vya Afya, Hospitali isomane - Dkt. Mollel