Beki Harry Maguire amefichua jinsi simu kutoka kwa David Beckham ilivyomsaidia kukabiliana na unyanyasaji kutoka kwa mashabiki, ambao wakati fulani umekuwa mbaya sana na familia yake ilikaa mbali na michezo.

Mchezaji huyo alistahamili usiku wa kustaajabisha kama mbadala wa kipindi cha pili katika ushindi wa 3-1 wa England dhidi ya Scotland mwezi uliopita, akishangiliwa na maelfu ya mashabiki wa nyumbani kabla ya kila mguso wake kukejeliwa ikiwamo bao la kujifunga la dakika ya 67.

Hapo awali Maguire alilengwa na mashabiki wa Arsenal wakati akiwakilisha Manchester United kwenye Uwanja wa Emirates na beki huyo wa kati amekabiliwa na shutuma nyingi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukosa nafasi chini ya Erik ten Hag pale Old Trafford.

Kocha wa England, Gareth Southgate alidai baada ya mechi ya Scotland, “Sijawahi kujua mchezaji anatendewa namna hii” na Maguire akafichua Beckham alimpigia simu siku chache baada ya mchezo huo na kumpa sapoti.

Beckham alivumilia hasira kali kutoka kwa mashabiki wa England waliokasirishwa na kadi nyekundu katika mechi ya mwaka 1998 ya Kombe la Dunia walipofungwa na Argentina.

Akizungumzia simu kutoka kwa Beckham, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 48, Maguire alisema: “Ilimaanisha kila kitu. Nimezungumza katika maisha yangu yote kuhusu David Beckham kuwa mtu niliyemtazama na kumtazama nilipokuwa mvulana mdogo.

Al Ahly waishtua Simba SC African Football League
Ukarabati Uwanja wa Mkapa bado kidogo tu!