Nahodha wa England Harry Kane anaamini kuwa, anaweza kucheza soka la ushindani hadi atakapofikisha umri wa miaka 40, huku akiahidi kutostaafu mapema katika timu ya taifa, lengo lake ni kuweka rekodi za mastaa kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Mshambuliaji huyo anejiunga na kikosi cha England ambacho kesho ljumaa (Oktoba 13) kina mchezo dhidi ya Australia na mechi ya kufuzu Euro 2024 dhidi ya Italia, juma lijalo.

Msimu huu ambao Kane amejiunga na FC Bayern Munich akitokea Tottenham, amefanikiwa kufunga mabao tisa na kutoa asisti tano katika mechi 10 za mashindano yote.

Kane mwenye miaka 30, alipoulizwa lini atastaafu soka timu ya taifa, alijibu: “Nimekuwa najivunia sana kuichezea England, hivyo kustaafu itakuwa ngumu, sijafikiria.

“Mimi ni mtu ambaye daima nitataka kuendelea kupambana ndani ya uwanja, nataka kuweka rekodi kama ambavyo wengine wameweka akiwemo Messi na Ronaldo.”

Ikumbukwe kuwa, Messi mwenye miaka 36, ameweka rekodi nyingi katika soka ikiwemo kushinda Ballon d’Or saba, huku Ronaldo mwenye miaka 38, akiwa na Ballon d’Or tano.

Pacome Zouzoua amtumia salamu Jean Baleke
Al Ahly waishtua Simba SC African Football League