Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’, imesema imeridishwa na mwenendo wa Ligi Kuu msimu huu 2023/04, ambayo sasa iko katika raundi ya tano na imesimama tena kupisha kalenda ya FIFA.

Ofisa Habari wa bodi hiyo, Karim Boimanda, amesema Ligi Kuu imekuwa na mvuto na ushindani mkubwa zaidi kuliko msimu uliopita.

Boimanda amesema pia viwango vya waamuzi wanaochezesha vimeongezeka ingawa amekiri kuna changamoto kwa baadhi yao, hivyo wataendelea kutoa semina kwa ajili ya kuboresha viwango vyao.

“Kwa tathmini ya haraka haraka mpaka kufikia raundi ya tano Ligi Kuu imekuwa ni mizunguko bora inayotupa ishara ya namna msimu huu 2023/24 utakavyokuwa,”

“Levo ya ushindani imekuwa kubwa sana kuliko tulivyotarajiwa, kwa hakika kabisa ukitazama michezo ambayo imefanyika, unaweza ukaona wazi kwa nini ligi hii inaimbwa na inaendelea kutangazika hapa Barani Afrika,” amesema Boimanda.

Ameongeza changamoto zilizotokea zitafanyiwa kazi na alifunguka kutegemea jicho la mwamuzi pekee si kitu rahisi sana na ndio sababu Ulaya walishaondoka na kuhamia katika matumizi ya VAR.

Moses Phiri achimba mkwara Ligi Kuu, Kimataifa
Ibrahim Class: Mpinzani wangu sio wa kumbeza