Serikali Nchini, imewataka Wafanyabiashara wa Madini kuwa wazalendo kwa kufuata taratibu zilizopo za ulipaji tozo, ada na kodi mbalimbali, ili kuiwezesha kupata mapato na kuendelea kuimarisha huduma kwa Wananchi ikiwemo ujenzi wa Barabara, Umeme, Afya na Elimu.

Hatua hiyo, inafuatia tukio la Serikali kupitia Wizara ya Madini kusimamisha leseni zote za Kampuni ya Nadoyoo Mineral Trading, kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa wahusika wa Kampuni hiyo akitorosha kilo 4.3 za Dhahabu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 562,288,207.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde mara baada ya kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo alisema atatenga siku na kukaa pamoja na Wafanyabiashara wa Madini, ili kujua changamoto inayopelekea baadhi yao kujihusisha na vitendo vya utoroshaji madini, hatua ambayo anaamini itasaidia uchukuaji wa njia sahihi za kushughulikia suala hilo.

“Mtu yeyote atayekamatwa kwa kosa la kutorosha madini, tutasimamisha leseni zake zote Nchi nzima wakati tukisubiri hukumu ya vyombo vya sheria na iwapo Mahakama itabaini mhusika ana hatia, tutachukua hatua kali ikiwemo kufuta kabisa leseni zote na kuhakikisha hatajihusisha tena na Biashara ya Madini Nchini.”

Mahakama yafuta kesi uingizaji, ulimaji mazao Kijenetiki
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 13, 2023